Thursday, May 5, 2011

Ni nini biashara yako?


                                    Ni  nini  biashara yako?
 Unaweza ukajibu swali hili kwa kuangalia vitu viafutavyo nini unazalish na kwa ajili ya nani?
Maana yake ni kuwa biashara ina mambo mawili
               Uzalishaji (Production)
               Masoko (Marketing)
Kitu cha msingi kukumbuka uko katika biashara ili kuzalisha /kutafuta pesa.
Maana yake ni kuwa lazima uwe na vitu vya kuuza na pia lazima uwe na watu wa kununua hivyo vitu vyako(kwa maana nyingine ni lazima uwe na bidhaa/huduma na pia wawepo wanunuzi wa bidhaa zako.)
 Kupata vitu unavyotaka kuuza unahitaji uzalishaji (bidhaa/huduma) na pia kutafuta  masoko ya kuuzia hizo bidhaa/huduma ulizozalisha.
Kwa hiyo biashara kwa maana nyingine ni bidhaa/huduma na masoko.
         Tuanze na uzalishaji (Production)
Mfano fikiria
Kama wewe ni mtengenezaji wa viatu/miwani ya jua, ukiulizwa biashara yoko ni nini , utasema ni  kutengeneza miwani /viatu.lakini hii ni biashara yako kweli?
Unachotengeneza ndicho unachauza?
Kama unatengeneza miwani ya jua ,kutengeneza miwani ya jua sio njia pekee ya kuelezea  uzalishaji wako.
Biashara yako ungeweza kuielezea kuwa ni kuzuia macho kupigwa na mionzi ya jua.
Kama utasema “nina biashara ya kutengeneza miwani ya jua” ni lazima utambue
Kuwa miwani ina vipande viwili vya plastiki vya rangi vilivyoshikwa na fremu za
Plastiki kwenye uso wako.
Hakuna mtu atakeye nunua miwani kwa kuwa anataka viande viwili vya plastiki/glasi vya rangi aviweke usoni mwake.
(HAPA NI LAZIMA UZALISHE ZAIDI YA MIWANI.) 
Unapoelezea biashara yako lazima pia uelezee kuhusu masoko yake
(It’s marketing) mfano ;ukisema biashara yako ni kuuza miwani kwa waitali.
Kumbuka biashara ni uzalishaji na masoko.
       Tuzumgumzie masoko (marketing)
“Utasema biashara yako ni biashara ya kutengeneza miwani za jua kwa waitalia”
Hii ni nzuri kidogo lakini kuna mamilioni ya waitalia , hakika huko katika biasha ra ya kuwatengenezea miwani za jua manilioni ya waitali wote.
  Fikiri biashara yako katika hali ya kwanini hawa watu wananunua miwani za jua?
   Hapa biashara yako itakuwa “kutengeneza miwani ya jua ambayo inazuia mionzi kwa ajili ya waitalia wanopenda usalama wa macho yao"
Mfano ukisema biashara yako ni kuzalisha fulana za kampuni ya ukwamba ;
Ukwamba akakupatia kila kitu (malighafi zote ) kwa ajili ya uzalishaji na aina ya fulana ,mfano na ukubwa wa hizo fulana. Hapa maana yake ni kwamba ukwamba anahitaji uweke gharama za uzalishaji tu hasa wafanya kazi (labour costs)
 Je unafikiri biashara yako ni nini?
Je kampuni ya ukwamba kiuhakika inanunua nini hasa kutoka kwako?
Je ni bei rahisi ya ufanyajikazi wako?(low cost of your labour).

Muhimu;
Kama hutasimamia vizuri bishara yako/kampuni yako au utachelewesha mzigo, mzigo ukawa chini ya kiwango,ukubwa tofauti, rangi  tofauti na mlivyokubaliana, Ukwamba hata nunua huduma toka kwako hata kama una bei rahiasi kuliko kampuni yoyote hapa duniani.
   Kutokana na maelezo hayo unaweza kusema biashara yako ni kutoa huduma (services) kuliko kutengeneza bidhaa.
Japokua unampatia ukwamba bidhaa za fulana,lakini ukwamba anapenda au anvutiwa na huduma yako ya usimamizi wa uzalishaji.
  Biashara yako hapa ni kuuza utaalam wako wa usimamizi wa uzalishaji kwa kampuni ya ukwamba.(selling production management skills)
“Unachozalisha kinaweza kuwa sicho unachokiuza”

Ili kufafanua vizuri kuhusu mada hiyo hapo juu hebu jaribu kufikiria kuhusu magazeti
Magazeti yanauza nini?
 Unaweza kufikiri na kusema kuwa magezeti yanauza habari kwa jamii,
Lakini jiulize mwenyewe kuuza magazeti kutaweza kuzalisha hela za kutosho kuendesh kampuni? Hela itakayopatikana haitoshi, kwani kuchapisha nakala moja
bei yake ni mara mbili ya bei ya kuuzia gazeti.
 Hapa makampuni ya magazetai yanauza nafasi za matangazo.
 Na ndio chanzo kikibwa cha mapato yao.
(They produce what they don’t sale and they sale what they don’t produce)

Muhimu;
Kama utashindwa kujua hasa kampuni yako iko katika biashara gani /inauza nini/
Inazalisha nini utakuwa umepoteza mwelekeo na hutatengeneza faida ambayo ndio msingi wa kuwa katika biashara (money making)

Hitimisho
1.       unachozalisha/unachotengeneza kinaweza kuwa sicho unachouza.
Kujua uko katika biashara gani au nini biashara yako lazima ufikirie haya; 
Kwa nini wananunua toka kwako?
2.     wakati unafikiria kuhusu  nani watanunua kutoka kwako ,fikiria pia kuhusu nani anahusika katika mafanikio yako ya kifedha ya kampuni
Watanzania wengi hatujui hasa ni nini biashara zetu(what is the business of your enterprise) hii inasababisha watu wengi sana kupata hasara na kufunga baadhi ya makampuni yao.

mtoi mc
ahsante sana
karibuni wadau wote kwa maoni na ushuri.
www. Biasharanikilimo.blogspot.com

Sunday, April 17, 2011

JINSI YA KUANZISHA BISHARA/MRADI( SOUND BUSINESS PLAN SHOULD CONTAIN THE FOLLOWING)

1.Utangulizi
  •     Jina na anwani ya biashara.
  •     Jina na anwani ya mmiliki.
  •     Asili ya biashara.
  •    Maelezo ya kifedha(statment of financing needed)
2 .Muhtasari wa biashara nzima(complete summary of your bisiness).
3.  Uchambuzi wa sekta ya biashara yako inakoenda(industry analysis)..
  •      Matazamio ya mbali na mwenendo wa sekta.
  •      Uchambuzi wa wapinzani wako katika biashara(analysis of competetors).
  •      Uawaji wa soko lako(marketing segmentation).
  •      Mfano; soko lako ni lipi (wototo, vijana, wazee nk
  •     Utabiri wa sekta(industry forecast)
4.Uchanganuzi wa biashara yako.(description of venture)
  •      Bidhaa
  •     Huduma
  •     Ukubwa wa biashara
  •     Mashine za ofisi na wafanyakazi
  •     Maelezo ya mjasilia mali( background of entrepreneur)
5.Pangalia juu ya uzalishaji wako
  •    Mashine na vyombo vitakavyotumika katika uzalishaji
  •    Majina ya watakaokupati/kuuzia malighafi kwa ajili ya ualishaji wako
6.Masoko.
  •       Bei
  •      Usambazaji
  •      Matangazo
  •      Wateja(customers).    
         

7.Pangalia jinsi biashara yailivyo
  •    Nani mmiliki wa biashara.
  •    Utambulisho wa washikadau wakubwa.
8.Tathimini mapungufu ya biashara yako.
  •     Zingatia mabadilikoa ya teknolojia
 9.Pangilia mfumo wa kifedha 
  •      Tabili utaingiza kiasi gani?
  •     Kiasi cha bidhaa kitakacho rudisha gharama zako za uzalishaji{ break even analysis}
  KARIBUNI WADAU WOTE WA BIASHARA, KILIMO, MIFUGO ,LISHE NA USHAURI.
 KWA MAWASILIANO PIGA No; 0713921703/2
 email:mtoimathias@rocketmail.com or mwinga21@yahoo.com
 

Saturday, April 9, 2011

UFUGAJI WA KUKU WA KISASA

                                                                                                           

               TARATIBU ZA KULEA VIFARANGA HADI KUUZA   
MATAYARISHO YA BANDA:
Safisha banda vizuri ndani na nje(anza kuondoa vumbi ndani , ukutani, na kisha fagia vizuri)
Kama ukiweza unaweza kupaka chokaa nyumba yote.
Acha chumba kikauke vizuri na kisha, weka  maranda/pumba za mpunga/maganda yakahawa nk.
Pulizia dawa yaani disnfectant(hapa ni vizuri ukapata ushauri)
UPOKEAJI WA VIFARANGA:
Katika chumba ulichoandaa tengeneza mviringo wa hard board kulingana na idadi ya vifaranga
weka karatasi juu ya tandiko kwa muda wa siku 4
tayarisha vyombo vya maji na chakula na uviweke ndani ya mviringo
weka taa za joto ndani ya huo mviringo
kwa madhumuni ya kuzuia upotevu wa joto funika mvirngo na asian cloth bila kuathiri mzunguko wa hewa.
kadri vifaranga vinavyokua ndio inabidi uongeza ukubwa wa mviringo. joto nani ya mviringo linatakiwe liwe
Upokeaji wa vifaranga
 Andaa daftari la kumbukumbu na hesabu vifafanga ulivyopokea. andika idadi ya waliokufa,vilema, vipofo. (count any deformity)
Viweke kwenye mviringo ulioandaa.
Hakikisha kuna mwanga wa kutosha.
Chunguza tabia za vifaranga kila mara

Mchoro ufuatao unaweza kukusaidia kutambua joto sahihi kwa vifaranga wako.
 Ufunguo: vidotidoti vinakilisha vifaranga
 
Too hot: Joto limezidi sana ,punguza joto
Too cold: Joto limepungua , ongeza joto
Correct: Joto sahihi kwa ajili ya vifaranga wako
AINA ZA CHAKULA NA MFUMO WA KULISHA:
KUKU WA NYAMA(broilers)
Broiler starter(wiki 3 za kanza)
Broiler finisher hadi kuuza.
NAMNA YA KUZUIYA MAGONJWA
Weka dawa ya kuua wadudu kwenye chimbo mlangoni ili watu waikanyage
(disinifectant +maji)
Punguza mwanga kwa kuku wanaokua
Wiki ya kwanza tumia dawa aina ya ANTIBIOTIC na VITAMIN kwenye maji
hapa ni vizuri ukapata ushauri

UTARATIBU WA CHANJO
Umri wa siku 3:  Gumboro
Umri wa siku7 :   Newcastle (kideri)
Umri wa wiki 2:  Gumboro

NAFASI YA KUKU WA MAYAI (STOKING RATE)
Mita moja ya mraba (m2): Inatosha kuku 9-12

MAGONJWA MENGINE YA KUKU NI KAMA
Coccidiosis ni ugonjwa unaosumbua sana kuku  na hutukea baada ya wiki 2 toka kuzaliwa
kukinga ni muhini hapa tafuta ushauri

  Picha ya kuku mwenye ugonjwa wa coccidoisis
         
Picha za kuku mwenye kideri(Newcastle diseases)

                             

                         


Ahsante  na karibu kwa ushauri pia karibu kwa  maoni
Mathias Mtoi
0713921703