Thursday, April 7, 2011

biashara ni kilimo

       Mapato ya binadam kwa sehemu kubwa yanatumika katika chakula(food).
Matumizi hayo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu;
1. kifungua kinywa(breakfast)
2.chakula cha mchana(lunch)
3.chakula cha jioni(dinner).
Chakula kinazalishwa na wakulima.
Chakula hiki kinaweza kutokana na vitu vifuatavyo;
Ngano
Mafuta-(alizeti,ufuta,nazi,karanga,mahindi,korosho,pamba,michikichi(miwese) ,sukar,mahindi,viungo(spicees)
Nyama (ng'ombe,mbuzi,kuku,bata,ngurure, kondoo),vitinguu,nyanya,pilipili,matango,maboga,majimb,viazi,matunda,mtana nk.
Ili kuweza kupata mahitaji haya lazima wawepo wadau /washiriki katika mchakato mzima wa kupata huduma au mahitaji.
               Kwa upande mmoja kuna mkulima/mzalishaji ambaye anazalisha ili kupata mahitaji yake muhimu ya kila siku kwa kuuza mifugo au mazao. Kitendo cha kubadilishana malighafi(mazao/mifugo) na pesa ni biashara.
"biashara" inahusiana na hali ya kuwa na shughuli ya kufanya aidha kama mtu binafsi au jamii kwa ujumla, kazi ambayo ina uasaidizi kiuchumi na kibiashara. Biashara ya mtu binafsi:Hii ni biashara inayomilikiwa na mtu mmoja. Mmiliki anaweza kuiendesha biashara hii yeye binafsi au pia anaweza kuwaajiri wafanyikazi kumsaidia. 
        Kwa upande mwingine hawa wakulima tunaweza kuwaita wafanyabiashara ya kilimo.
 Biashara ya kilimo hasa kuzalisha ni nzuari kuliko kuwa mchuuzi wa bidhaa za wenzetu.
kilimo ni eneo ambalo lina soko la kuyosha nawatu wengi hasa watanzania nawashauri wawekeze kwenye kilimo.
Tutajitahidi kutoa ushauri wa kilimo cha biashara kwenye hii blog. kwa kadri mungu atakavyotubariki.
 Ahsante
mathias c mtoi
-Diploma in Animal Production(DAP)
-Advanced Diploma in Business Adminstration(ADBA)
-Postgraduate in International Business Management(PGDIBM)

No comments:

Post a Comment