Saturday, April 9, 2011

UFUGAJI WA KUKU WA KISASA

                                                                                                           

               TARATIBU ZA KULEA VIFARANGA HADI KUUZA   
MATAYARISHO YA BANDA:
Safisha banda vizuri ndani na nje(anza kuondoa vumbi ndani , ukutani, na kisha fagia vizuri)
Kama ukiweza unaweza kupaka chokaa nyumba yote.
Acha chumba kikauke vizuri na kisha, weka  maranda/pumba za mpunga/maganda yakahawa nk.
Pulizia dawa yaani disnfectant(hapa ni vizuri ukapata ushauri)
UPOKEAJI WA VIFARANGA:
Katika chumba ulichoandaa tengeneza mviringo wa hard board kulingana na idadi ya vifaranga
weka karatasi juu ya tandiko kwa muda wa siku 4
tayarisha vyombo vya maji na chakula na uviweke ndani ya mviringo
weka taa za joto ndani ya huo mviringo
kwa madhumuni ya kuzuia upotevu wa joto funika mvirngo na asian cloth bila kuathiri mzunguko wa hewa.
kadri vifaranga vinavyokua ndio inabidi uongeza ukubwa wa mviringo. joto nani ya mviringo linatakiwe liwe
Upokeaji wa vifaranga
 Andaa daftari la kumbukumbu na hesabu vifafanga ulivyopokea. andika idadi ya waliokufa,vilema, vipofo. (count any deformity)
Viweke kwenye mviringo ulioandaa.
Hakikisha kuna mwanga wa kutosha.
Chunguza tabia za vifaranga kila mara

Mchoro ufuatao unaweza kukusaidia kutambua joto sahihi kwa vifaranga wako.
 Ufunguo: vidotidoti vinakilisha vifaranga
 
Too hot: Joto limezidi sana ,punguza joto
Too cold: Joto limepungua , ongeza joto
Correct: Joto sahihi kwa ajili ya vifaranga wako
AINA ZA CHAKULA NA MFUMO WA KULISHA:
KUKU WA NYAMA(broilers)
Broiler starter(wiki 3 za kanza)
Broiler finisher hadi kuuza.
NAMNA YA KUZUIYA MAGONJWA
Weka dawa ya kuua wadudu kwenye chimbo mlangoni ili watu waikanyage
(disinifectant +maji)
Punguza mwanga kwa kuku wanaokua
Wiki ya kwanza tumia dawa aina ya ANTIBIOTIC na VITAMIN kwenye maji
hapa ni vizuri ukapata ushauri

UTARATIBU WA CHANJO
Umri wa siku 3:  Gumboro
Umri wa siku7 :   Newcastle (kideri)
Umri wa wiki 2:  Gumboro

NAFASI YA KUKU WA MAYAI (STOKING RATE)
Mita moja ya mraba (m2): Inatosha kuku 9-12

MAGONJWA MENGINE YA KUKU NI KAMA
Coccidiosis ni ugonjwa unaosumbua sana kuku  na hutukea baada ya wiki 2 toka kuzaliwa
kukinga ni muhini hapa tafuta ushauri

  Picha ya kuku mwenye ugonjwa wa coccidoisis
         
Picha za kuku mwenye kideri(Newcastle diseases)

                             

                         


Ahsante  na karibu kwa ushauri pia karibu kwa  maoni
Mathias Mtoi
0713921703

8 comments: